Baraza la Wazee wa Klabu ya Simba wamesema kuwa hawako tayari kufanya mabadiliko yoyote katika Klabu hiyo mpaka pale watakapojua hatma ya viongozi wao walioko rumande hivyo hawapo tayari kuona mtu yeyote kuingilia mfumo uendeshaji wa timu hiyo.

Wamefikia hatua hiyo mara baada ya baadhi ya wanachama wa Klabu hiyo kuitisha mkutano wa kutaka kufanya mabadiliko mbalimbali wa namna ya uendeshaji wa Klabu hiyo ya Simba huku wakipinga ajenda zilizoandaliwa.

Aidha, Wazee hao wamesema kuwa mkutano ulioandaliwa ni batili kwani viongozi wa ngazi za juu hawajahusishwa kwakuwa wako rumande wakikabiliwa na kesi ya kujibu, hivyo hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kuandaa mkutano wenye lengo la kufanya mabadiliko.

Manny Pacquiao ataka kujiunga na vikosi vinavyopigana na magaidi wa ISIS
Majaliwa awaasa watumishi wanaofanyakazi viwandani