Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi, Richard M. Kayombo ametangaza rasmi kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanzisha kampeni kabambe ya kutoa msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma.

Lengo likiwa ni kuongeza urahisi wa kulipa madeni ambayo yalikuwa kikwazo kwa wafanyabiashara wengi na hata kuendelea na biashara zao.

Hivyo amewaomba wote wenye malimbikizo ya nyuma wajitokeze na kufika katika ofisi za TRA, ili kuweza kuweka ombi la kupata msamaha wa malimbikizo ya riba na adhabu.

Amezungumza hayo leo na vyombo vya habari pindi alipokuwa akitoa ripoti ya makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo mapato hayo yameongezeka kwa asilimia 7.5 kulinganisha na mapato yaliyokusanywa mwaka jana.

Aidha amewaomba walipa kodi wote kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kujenga utamaduni wa kudai Risiti za kielektroniki za kutolea risiti (EFD,s) kwa wafanyabiashara.

Bofya video hapa chini kumsikiliza Kayombo akitangaza rasmi kampeni kabambe ya kusamehe madeni na malimbikizo ya kodi.

Video: Wema Sepetu awaomba watanzania wamuombee
Video: TRA yafunguka makusanyo ya kodi mwaka wa fedha 2017/18

Comments

comments