kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Shirika la habari la Ufaransa AFP, zimeeleza watu takribani milioni tatu duniani wameambukizwa virusi vya corona huku karibu asilimia 80 wametoka Ulaya na Marekani

Kwa namba halisi takwimu hizo zinaeleza takribani maambukizi 3,003,344 yamebainika, ikiwemo vifo 209,388, na vingi vya hivyo vimetokea Ulaya ambako kuna jumla ya maambukizi 1,393,779 na vifo 126,233.

Marekani ambako janga la virusi vya corona linasambaa kwa kasi kuna maambukizi 980,008 vikiwemo vifo 55,637.

Hata hivyo idadi ya maambukizi yaliyogunduliwa inaaminika kuwakilisha sehemu tu ya idadi ya kweli ya maambukizo ya watu waliopimwa kwa sababu nchi nyingi hazijafanya vipimo kwa kiwango cha juu.

Wakenya 18 wafia nje ya nchi kwa Corona
FIFA yapendekeza kanuni mpya