Kikosi cha Esperance de Tunis ya Tunisia kinatarajiwa kuwasili nchini leo Ijumaa kwa ndege ya kukodi tayari kwa mchezo dhidi ya Azam FC huku idadi ya watu katika msafara wao ikificha.

Azam FC wanatarajia kuvaana na Esperance katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, keshokutwa Jumapili.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saadi Kawemba, amesema wapinzani wao hao watatua leo usiku na kufikia katika Hoteli ya Bahari Beach.

“Hawajatutaarifu watakuja na kikosi cha watu wangapi kwa kuwa watajihudumia wenyewe,” alisema Kawemba ambaye juma lililopita alisema kuwa Esperance wakifika wao kama Azam FC watawahudumia kila kitu kwa kuwa wamekubaliana makubaliano maalum ili nao wakienda Tunisia wawahudumie pia.

Thiago Silva Asikitishwa Na Maamuzi Ya Man City
Mbeya City Waanza Safari Ya Kuwafuata JKT Mgambo