Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imewaonya Wasanii wa Tanzania wanaohamasisha matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi kupitia tungo za nyimbo zao, na kudai kuwa itawachukuliwa sheria dhidi ya vitendo hivyo.

Onyo hilo limetolewa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya wakati akiongea na Waandhishi wa Habari hii le Desemba 7, 2022 jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya.

Amesema, “Kuna Wasanii wanahamasisha matumizi ya Dawa za Kulevya ikiwemo bangi, kama wanadhani badala ya kutunga nyimbo za kuhamasisha Jamii wao wanatunga nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya, tutawachukulia hatua.”

Kamishna Jenerali Kusaya ameongeza kuwa, “Kama kuna Msanii anadhani anaweza kupata umaarufu kwa kupitia nyimbo za kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya hatutomuacha, sheria itachukua mkondo na ipo siku nitawaita ili muone kitu gani tumekifanya kwa Wasanii wanaotaka kupata umaarufu kwa kutumia Dawa za Kulevya.”

Mgunda ataja mbinu mpya Ligi Kuu
Eden Hazard ajiweka pembeni Ubelgiji