Leo Shirika la bima ya Afya limezindua kampeni  ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kadi ya bima ya afya, ambapo kila mtanzania atapata bima hiyo kupitia mchezo wa bahati na sibu utaochezwa kwa miamala ya simu.

Taasisi ya Nordic Foundation Tanzania NOFOTA  imeratibu kampeni hiyo itayoanzia katika jiji la Dar es salaam na kuenea katika mikoa  yote nchini lengo lilikwa kutoa fursa kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya.

Katika kampeni hiyo kutatolewa kadi 10 za bima ya afya kwa kila mwananchi wa jiji la Dar es salaam, itakayowezesha kutoa huduma kwa familia nzima ndani ya mwaka mmoja.

Daktari bingwa wa upasuaji na mwelekezi utoaji huduma ya bima ya afya, Respicius Salvatory, amesema kupitia mchezo wa kubahatisha wa kupata kadi ya bima ya afya, wamekusudia kufikia kila mwananchi ili kuondokana na gharama nyingi wanazokutana nazo pindi wanapokumbwa na maradhi.

Salvatory amesema 73% ya watanzania hawatumii kadi ya bima ya afya kutokana na kutokuwa na elimu, hivyo kupitia 500 watachezesha mchezo wa kubahatisha kwa kila mwananchi kupitia simu yake ya mkononi ili kujipatia kadi  kwa taratibu pendekezwa.

Huduma hiyo imeamriwa kutolewa baada ya watanzania wengi kupoteza maisha yao kwa kukosa fedha za kukimu huduma za hospitali.

Korea Kaskazini kufanya majairibio zaidi ya makombora
Kweli Arsenal wana mkosi, Sanchez aumia tena