Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt. Vicent Anney amesema watu wawili wameuawa  akiwemo hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Handeni, Joachim Mwakyoma baada ya kupigwa na  wananchi wenye hasira.

Dkt. Anney amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa kitendo cha hakimu na wenzake kuingia katika shamba hilo kiliwashtua wananchi waliowafuata na kuwahoji na yakaibuka malumbano.

Kwa mujibu wa Gazeti la mwananchi Dkt. Anney amesema tukio hilo limetolea katika kijiji cha kibole kilichopo Halmashauri ya Busokelo.

Amesema, Hakimu huyo alikuwa ameambatana na wenzake wawili kwenda kwenye shamba lenye mgogoro na wanakijiji walishinda kesi katika  Mahakamani Kuu  Desemba mwaka 2022  baada ya kesi hiyo kusikilizwa mahakamani kwa miaka zaidi ya 10.

Ameongeza kuwa, tukio hilo wananchi wawili walipigwa risasi  na mmoja wa watu waliokuwa wameambata na hakimu na  walikimbizwa  katika hosptali ya Itete kwa matibabu zaidi na hali zao zinaendelea vizuri 

“Kwa sasa tumeliachia Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi, Wilaya hii imekithiri matukio ya mauaji yanayohusiana na migogoro ya ardhi, tunaendelea kushughulikia kwa kushirikisha na  viongozi wa dini, kamati za amani wilaya kuona wanakemea  na kutoa elimu kwa jamii kuachana na tabia ya kuchukia sheria mkononi.” Amesema Dkt. Anney.

Ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere wafikia asilimia 80.22
Wingu jeusi lazidi kumsogelea Biden