Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amewaonya wazazi wanaozembea kwenye malezi na hivyo kuzalisha watoto wahalifu.

Waziri Gwajima amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Mbezi Luisi kuelekea Siku ya Familia inayoadhimishwa ifikapo Mei 15 ya kila mwaka.

Amesema kuwa wakati Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji watu 31 waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na na vitendo vya kihalifu maarufu ‘Panya Road’, wizara yake itafanya uchunguzi wake ili kubaini kama kuna wazazi wanahusika kwa namna moja au nyingine na matukio yanayofanywa na watoto wao.

“Hili ni tatizo linalotokana na wazazi, mtoto haonekani na mzazi hahangaiki kumtafuta. Upo uwezekano wa baadhi ya watoto kutumwa na wazazi au kufundishwa,” alisema Dk Gwajima.

Itakumbukwa Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema watu 31 walikamatwa katika operesheni maalumu ya msako wa mtaa kwa mtaa, dhidi ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.

Ambapo alaisema kuwa kati ya watu waliokamatwa ni vijana kati ya miaka 13 hadi 20, ambao hutumia mapanga, visu, nondo na mikasi mikubwa wanapofanya uhalifu.

Simulizi: Siri za wafanyabiashara
Habari kubwa kwenye Magazeti leo Mei 9, 2022