Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji nchini, Angellah Kairuki ameeleza kuridhishwa na hatua za uwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula cha MAGIN kilichopo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kwa kuwa na mitambo yenye ubora na chenye nia ya kuzalisha mafuta kwa tija nchini.

Ameeleza hayo jana lipotembelea maeneo ya uwekezaji katika wilaya za mkoa wa Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake katika mkoa huo ili kujionea mazingira ya wawekezaji nchini, kusikiliza na kutatua kero zao.

Waziri Kairuki amekipongeza kiwanda hicho kuzalisha mafuta yenye ubora na kupatikana kwa urahisi kwa kuzingatia uwepo wa malighafi za kutosha zinapatikana nchini na kueleza imeongea motisha kwa wawekezaji hao.

 “Ninawapongeza kuona fursa ya kuwekeza katika mafuta ya kula na hii ni sahihi kwa kuzingatia ukanda huu una alizeti nyingi na kuwa na uhakika wa malighafi ya uzalishaji,” Amesema Kairuki

Ameeleza kuwa uamuzi wa kuwekeza katika mafuta ni sahihi kwani taifa limekuwa likipoteza zaidi ya shilingi Bilioni 443  kwa mwaka kwa uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchi.

“Kama nchi tumekuwa tukizalisha mafuta kwa asilimia 40 tu na alilimia 60 kuagiza mafuta kutoka nje ambapo imekuwa ikitumia fedha nyingi, uwepo wa kiwanda hiki utasaidia kuokoa fedha hizo na kuongeza tija katika uchumi wa taifa letu,” Ameongeza Waziri Kairuki

Aidha, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuweka nafuu za kikodi kwa wawekezaji ili kuziangalia sekta zenye upungufu ikiwemo ya mafuta ya kula na sukari, na kuendelea kutoa rai kwa benki kuendelea kusaidia vyama vya wakulima kuhakikisha kunakuwa na mnyororo wa thamani katika sekta ya uwekezaji nchini.

Dk. Abbas: Timu zianze mazoezi
Bendera ya Marekani yashushwa nusu mlingoti, maombolezo vifo vya corona

Comments

comments