Kapteni mstaafu George Mkuchika ameapishwa kuwa Waziri ndani ya ofisi ya Rais Kazi Maalum leo Jumatano Juni 2, 2021, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Mkuchika amekula kiapo hicho mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kutoonekana hadharani kwa takriban miezi mitatu.

Awali Mkuchika alikuwa Waziri wa Utumishi na Utawala Bora nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Mohamed Mchengerwa.

Mkuchika alihamishwa kwenye wizara hiyo kufuatia mabadiliko ya baraza la Mawaziri aliyofanya Rais Samia Machi 31, 2021.

Hata hivyo Mkuchika hakuwepo siku ambayo Mawaziri waliapishwa na baadaye ikaelezwa kuwa ni mgonjwa.

Jenerali wa Uganda aliyepigwa risasi azungumza
Majaliwa awataka Makatibu Tawala kuhakikisha miradi inawafikia wananchi