Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Ummy Mwalimu amewaagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuacha kukaa ofisini na kutembelea maeneo ya vijijini kutatua na changamoto.

Ametoa agizo hilo leo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ya Katuna, Halmashauri ya Wilaya Tanganyika Mkoani Katavi kwa lengo la kujua changamoto zinazozikabili Halmashauri zilizopo pembezoni.

Amesema kuwa TARURA makao makuu wanatakiwa kutoka ofisini watembelee vijijini kujua maeneo ambayo yanachangamoto ya miundombinu ili kuweza kutoa vipaombele zaidi wakati wa kupanga bajeti za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara nchini.

“Haiwezekani TARURA mkakaa ofisini wakati matatizo mengi yanapatikana kwa wananchi hasa wale wanaokaa pembezoni, nawaagiza kuanzia sasa waache kukaa ofisini watoke na kwenda ‘site’ kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hasa katika maeneo ya vijijini,” amesema Waziri Ummy

Alisema kwa sasa Serikali imejiwekea mkakati wa kuhakikisha inatatua changamoto za miundombinu ya barabara vijijini.

TRC yatia saini mkataba ununuzi wa vichwa 17 vya treni
Nauli hazijapanda - LATRA