Mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amepinga kauli za rais wa Marekani, Dolnad Trump huku akitaka kuwepo kwa umoja, na kusitishwa kwa siasa katika mlipuko wa virusi vya Corona.

Rais Trump alionya kwamba atafikiria kusitisha ufadhili dhidi ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa, akilishutumu kuipendelea China na kudai walilisaidia sana taifa hilo.

Dkt. Tedros amepinga kauli za Trump akisisitiza kuwa: ‘Tunasaidia kila taifa ,hatuna upendeleo wowote’.

“Tusitumie Covid kisiasa…, Tuwe na uaminifu na umoja . Na uongozi wa uaminifu kutoka Marekani na China. Vitu muhimu vipewe kipaombele na tafadhalini wekeni siasa karantini”. Amesema Dkt. Tedros.

Aidha, akijibu maswali katika mkutano na vyombo vya habari siku ya Jumatano, waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba utawala wa Trump utaangazia upya ufadhili kwa shirika hilo.

”Mashirika lazima yafanye kazi. lazima kazi zao zionyeshe matunda”, alisema Pompeo.

Awali mshauri wa mkuu wa WHO alisema kwamba ushirikiano wao wa karibu na China ulikuwa wa kufana katika kuelewa ugonjwa huo katika hatua zake za kwanza.

Shambulio la Rais Trump dhidi ya WHO linajiri wakati ambapo amekuwa akiukosoa utawala wa Dkt. Tedros kwa jinsi unavyolichukulia janga hilo nchini Marekani.

Mkude ahofia viwango vya wachezaji
Reliants Lusajo: Elimu yangu ina msaada mkubwa Namungo FC

Comments

comments