Jana Nigeria ilikuwa na mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya Wizkid kulazimika kumchana Seyi Shay kupitia Tweeter baada ya kudai kuwa anajua yeye ndiye aliyemuandikia Drake wimbo wake wa ‘One Dance’.

Seyi-Shay

Sey Shay

Sey Shay alichafua hali ya hewa baada ya kufanya mahojiano na Onstage TV na kueleza kuwa anajua wimbo huo uliandikwa na Wizkid na kwamba hata mdundo wa wimbo huo ni wa Legendary Beatz kwa kushirikiana na watayarishaji wengine wa muziki.

Haikuchukua dakika nyingi kabla ya Wizkid kumtaka asiongelee asilolijua ‘funga mdomo wako’ kupitia Twitter na pia kumjibu shabiki aliyeuliza kama maaelezo ya Sey Shay yana ukweli. “Alidanganya,” aliandika Wizkd kwa kiingereza.

Hata hivyo, baada ya kumchana, Sey Shey alirudi nyuma na kueleza kuwa alitoa taarifa hizo kimakosa kwa sababu aliamini ‘mambo ya kusikia’ na akamuomba radhi Wizkid. Mrembo huyo anayeaminika aliwahi kuwa na uhusiano na Wizkid alieleza kuwa lengo lilikuwa kumtetea Wizkid.

TWEET

Wawili hao walielewana na kusafisha hewa iliyokuwa imeanza kutishia urafiki wa Wizkid na wasanii wakubwa wa Marekani akiwemo Drake. Drake alishiriki kwenye remix ya Ojuelegba ya Wizkid na kumshirikisha pia kwenye albam yake.

Sio Sey Shey peke yake ambaye alikuwa amepotoshwa, wiki chache zilizopita, rapa wa Marekani mwenye asili ya Nigeria, Wale alisema kuwa anaamini kuwa wimbo ule wa Drake ni wimbo wa Wizkid kwa kuusikiliza tu midundo pamoja na uimbaji wake.

Video: Bilioni 2.5 imetengewa Morogoro ujenzi wa Hospitali
DRFA Washangazwa Na Maamuzi Ya TFF