Kiungo wa klabu ya Man city Yaya Toure, ameibuka na kumkandia mwamuzi Andre Marriner kwa madai aliwaminya katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ambapo waliambulia sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Tottenham Hotspur.

Toure, amesema walistahili kushinda mchezo huo, endapo haki ingetendeka, lakini mwamuzi Marriner alishindwa kuzitumikia vyema sheria 17 za soka, na hatimae wakaambulia matokeo yaliyowapa point moja.

Kiungo huyo kutoka Ivory Coast, amesema wakati Man City wakiongoza mabao 2-1, beki wa kulia wa Tottenham Kyle Walker alimgonga kwa makusudi Raheem Sterling katika eneo la hatari, lakini mwamuzi huyo alijifanya hakuona kosa hilo, ambalo kwake aliamini lilikua ni penati.

Tokeo la picha la Yaya Toure: Raheem Sterling was too honest - he should have gone downKyle Walker (kushoto) akipambana na Raheem Sterling.

Amesema baada ya kitendo hicho kutokea, dakika moja baadae Spurs walifanikiwa kupata bao la kusawazisha.

“Tunajihisi kukosewa na mwamuzi Marriner, hakututendea haki, ilikua penati halali na kila mmoja aliona,”Amesema Toure. “ulikua mchezo mzuri kwetu na tulipaswa kushinda.

“Baada ya mchezo, kila mmoja wetu alijihisi vibaya, maana meneja alitaka kuona lengo la ushindi linatimia.

Sare ya mabao mawili kwa mawili imeifanya Man City kukaa katika nafasi ya tano, kwenye msimamo wa ligi ya nchini England (PL) kwa kufikisha  point 43.

Arsene Wenger Aomba Radhi
Jammeh aondoka na mamilioni Gambia, aiacha hazina tupu