Uongozi wa Yanga umesema unalifanyia kazi suala la wachezaji wao kugoma kufanya mazoezi kwa madai ya kudai mishahara yao.
Wachezaji wa Yanga, jana waligoma kufanya mazoezi kwa madai ya kutolipwa mshahara wao wa Novemba, mwaka huu.
Jana zilifanyika juhudi za kumpata Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, bila ya mafanikio.
Lakini leo, Baraka amezungumza na Dar24 na kusema wanalifanyia kazi suala hilo.
“Ni suala kati yetu na wao, sasa uongozi unalifanyia kazi na litamalizika.
“Ninaamini leo utawaona mazoezini, kesho na hata kwenye mechi utaendelea kuwaona,” alisema.
Wachezaji wa Yanga, jana walifika kwenye Uwanja wa Uhuru pamoja na makocha wote tayari kwa mazoezini.
Lakini wakiwa pale, waligoma kuingia uwanjani (kwenye pitch) kuanza mazoezini na baadaye ilielezwa walikuwa wakidai mshahara wao.
Hali hiyo ilizidi kuwa mbaya baada ya wachezaji kuamua kuondoka mazoezini.

Trump afunguliwa mlango rasmi kuingia ‘White House’
Leicester City waipeleka kadi ya Vardy mbele ya FA