Klabu ya Young Africans imeachana rasmi na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza kwa makubaliano ya pande mbili.

Young Africans imeachana na Mshambuliaji huyo kwa ghafla sana, tofauti na wachezaji wengine ambao wameachwa, ambapo taarifa zao za kuondoka klabuni hapo zilifahamika kitambo.

Baada ya kuachana na Young Africans, Ntibazonkiza mwenye umri wa miaka 34 amesema klabu hiyo inaongozwa kiinyeji na haina watu sahihi wa tiba.

Kauli hiyo inaonyesha huenda kulikua na msigano kati ya Mshambuliaji huyo na viongozi pamoja na jopo la madaktari (tiba).

Ntibazonkiza alisajiliwa Young Africans siku moja baada ya kuifunga Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwaka 2020, Uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Alianza kuitumikia klabu hiyo baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili mwezi Januari, kwa kushiriki michuano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Ntibazonkiza anakua mchezaji wapili wa kimataifa kuachwa na Young Africans katika kipindi hiki akitanguliwa na beki kutoka Ghana Lamine Moro.

Jitu la Azam FC hili hapa!
Serikali ya Zanzibar yaapa kuulinda Muungano