Kikosi cha Young Africans kimewasili salama jijini Mwanza mapema leo Alhamis (Januari 27) asubuhi, tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Mbao FC.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa CCM Kirumba keshokutwa Jumamosi (Januari 29), ukihamishwa kutoka Uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Young Africans inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 35 imewasili jijini humo na kupokewa kwa shangwe na Mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege.

Wakati huo huo Benchi la Ufundi la Young Africans limethibitisha nyota kadhaa watakaoukosa mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Mbao FC.

Wachezaji Djuma Shabani na Yannick Bangala wamejiunga na timu ya Taifa ya DR Congo huku Mzee wa kuwajaza Heritier Makambo akiwa ameomba ruhusa, Daktari wa Football Khalid Aucho atakua nje ya uwanja kwa sababu ya kadi za njano.

Wengine ni Viungo wa wawili ambao ni Majeruhi Feisal Salum na Denis Nkane.

Katika hatua nyingine Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amesema Kocha Msaidizi Cedric Kaze ameomba ruhusa hivyo naye hatakua sehemu ya Mchezo huo.

Rais Samia:Tufanye kazi kwa bidii
Uchaguzi Kenya 2022:Muunganiko wa Ruto na Mudavadi una tija?