Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, ameagiza kukamatwa kwa watumishi sita wa kituo cha pamoja cha forodha ili wahojiwe kwa tuhuma za rushwa sambamba na wananchi wengine watano waliokuwa wakiwapokelea fedha hizo.

Akizungumza na Watumishi wa kituo hicho hii leo Septemba 8, 2022, Chalamila amesema Agosti 29, 2022 iliundwa kamati ya kuchunguza mwenendo wa usafirishaji wa mazao toka Tanzania kwenda Uganda, na kubaini uwepo wa baadhi ya watumishi wasio waadilifu.

Amesema, “Iligundulika baadhi ya watu kuwa na nyaraka feki ambazo zinatumika kugongwa mihuri kwa kushirikiana na maafisa wa kituo hicho cha forodha na wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Kufuatia hatua hiyo, Chalamila ameliagiza Jeshi la polisi na TAKUKURU Mkoa wa Kagera, kuwakamata na kuwachunguza watumishi waliotajwa kwenye ripoti ya wakiwemo na mawakala waliokuwa wakitumika kuwapokelea fedha na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa pia amemuagiza Kaimu Meneja wa TRA Kagera, kufanya mabadiriko katika kituo hicho pamoja na taasisi nyingine zinazohusika huku akiwataja wanaotakiwa kukamatwa na kuhojiwa ni Maandalio Simon, Mzakiru Kachwamba na Anacreth Thedei wote kutoka idara ya kilimo, na Faudhi Msafiri, Aloyce Matiku na Geoge Adrof kutoka idara ya Mionzi.

Wengine ni Khadija Athuman, Restuta Peter, Sam Julias, Samora Elias na Devota Rutaselo ambao ni wananchi wa kawaida waliokuwa wakitumiwa na watumishi kupokea fedha kama mawakala wao huku akisema na kutoa onyo kali kwa watumishi wengine.

Hata hivyo, Chalamila amemtaka Kaimu Meneja wa TRA kagera kuendeleza ufuatiliaji katika mipaka ya Rusumo, Kabanga na Mrongo ili kuwabaini watumishi wasio wazalendo ambapo Katibu Tawala Mkoa wa Kagera amesema kituo hicho kimegubikwa na urasimu unaopelekea mapato ya Serikai kupotea.

Kukamatwa kwa watu hao, kunafuatia Jeshi la polisi Mkoani Kagera, kutoa taarifa ya kumkamata raia wa Uganda aliyekutwa na mihuri mitatu ya idara tofauti za Tanzania Septembar 6, 2022 akidaiwa kugonga vibali vya wafanyabiashara, wana

Majaliwa aagiza wahusika ujenzi Chuo cha Veta wakamatwe
Wasimamizi ujenzi VETA washukiwa ubadhilifu