Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa mzunguuko wa tatu wa Kundi J wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Benin.

Stars itakuwa mwenyeji wa Benin Alkhamis (Oktoba 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikianza maandalizi rasmi jana Jumatatu (Oktoba 04), uwanjani hapo.

Mpaka leo Jumanne (Oktoba 05) majira ya asubihi wachezaji 18, ndio walikua wameripoti kambini kuendelea na mazoezi chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen, ambaye ana jukumu la kuifikisha Stars kwenye Fainali za Kombe la Dunia zitakazounguruma nchini Qatar mwaka 2022.

Wachezaji walioripoti kambini hadi sasa upande wa Walinda Lango ni: Ramadhan Kabwili, Metacha Mnata, Aishi Manula na Wilbol Maseke

Mabeki: Kibwana Shomari, Edward Manyama, Kenedy Juma, Mohamed Hussein, Dickson Job na Nickson Kibabage.

Viungo: Ibrahim Sopu, Mzamiru Yassin, Feisal Salum na Idd Seleman

Washambuliaji: John Bocco, Kibu Denis, Meshack Abraham na Relliants Lusajo

Chelsea yamshangaza Antonio Conte
Masha: Nimeombwa kugombea tena Nyamagana, kuna fitna...