Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Regine Hess Balozi anayeiwakilisha Ujerumani nchini Tanzania, ambaye anamaliza muda wake wa utumishi nchini.

Katika mazungumzo yao, yamegusia ushirikiano uliopo katika sekta afya, maji, michezo, ulinzi, uwekezaji na utalii kati ya Ujerumani na Zanzibar.

Aidha, Balozi Hess ampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuunda kamati ya maridhiano kitaifa kati ya Chama cha CCM na ACT Wazalendo.

Balozi Hess pia amemtambulisha Balozi mdogo wa Ujerumani atakayefanya kazi zake Zanzibar, Dkt. Jenny Bouraima kwa Rais Dk.Mwinyi.

Eden Hazard kufanya maamuzi magumu
Hassan Maulid awaangukia mashabiki Mbeya City