Harold Edward Holt, 1908–67
Harold Edward Holt mzaliwa Sydney Nchini Australia mwaka wa 1908 ambaye safari yake ya maisha kisiasa ilianza baada ya kuhitimisha maisha ya kielimu na kumfanya achaguliwe kuwa Kiongozi wa Shirikisho cha Fawkner mwaka wa 1935.
Alipata kuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa Chama cha Liberal baada ya kustaafu kwa Sir Robert Menzies Januari 1966 na muda wake kama Waziri Mkuu uliungwaji mkono na Taifa la Marekani katika vita vya Vietnam, akipata ushindi wa kushangaza wa uchaguzi wa 1966 kwenye jukwaa la pro-Vietnam.
Kutoweka.
Harold Holt alitoweka alipokuwa akiogelea kwenye Ufukwe wa Cheviot karibu na Portsea, Victoria Desemba 17, 1967 na Mwili wake haukupatikana tena.
Bila kubainisha sababu ya kifo cha Holt, ripoti ya pamoja ya Polisi wa Jumuiya ya Madola na Victoria, iliyowasilishwa Januari 1968, ilihitimisha kwamba, ‘… hakujawa na dalili kwamba kutoweka kwa marehemu Holt kulikuwa jambo lingine isipokuwa kwa bahati mbaya’.
Ripoti hiyo, iligundua kuwa harakati zake za mwisho zilifuata mtindo wa kawaida wa nyumbani, mwenendo wake ulikuwa wa kawaida na licha ya ujuzi wake wa ufuo, hali ya msukosuko (pepo kali, bahari mbaya na mafuriko), kwamba vilimshinda.
Maelezo yaliyotolewa kwa kushindwa kuupata mwili huo, ni pamoja na kushambuliwa na viumbe vya baharini, mwili huo kupelekwa baharini na mawimbi au kukwama kwenye miamba.
Ingawa nadharia mbalimbali zimefafanuliwa kuhusu kutoweka kwa Holt, Serikali ya Jumuiya ya Madola haikuona uchunguzi rasmi kuwa muhimu, ikikubali hitimisho la ripoti ya Polisi kuwa alipotea na hakuonekana.
Rekodi.
Hifadhi ya Taifa ina kumbukumbu mbalimbali zinazohusiana na kutoweka kwa Holt, na matukio yaliyofuata mara moja: utafutaji usio na mafanikio wa mwili wake; ibada za kumbukumbu na maombolezo ya kuondokewa na kiongozi wa kitaifa.
Uwaziri Mkuu wa muda wa John McEwen; na uteuzi wa mbadala wa Holt. Mifano ya aina za kumbukumbu zilizoshikiliwa ziliorodheshwa, sipokuwa zile zilizooneshwa vinginevyo na zinazotunzwa na Kumbukumbu za Kitaifa huko Canberra.
Utafutaji.
Wakati wakiendela kumtafuta, mkoba wa Holt ulipatikana, hapo wakapata ufahamu kuhusu kazi yake wakati alipotoweka, ni filamu ya kimya iliyofanywa na Polisi wa Victoria ikiigiza upya mienendo ya mashahidi kwenye Ufukwe wa Cheviot na hali ambazo Holt alikutana nazo.
Faili muhimu la Idara ya Waziri Mkuu (A1209, 1968/8063), iliyo na ripoti za Polisi, mawasiliano, ramani, picha, taarifa kwa vyombo vya habari na hati zinazopendekeza taarifa muhimu zilizozuiliwa ili kusaidia utoaji wa taarifa kamili ya matukio.
Tetesi.
Mengi yaliongelewa wengine wakisema huenda Holt aliliwa na papa au labda aliuawa na mawakala wa siri kutoka Umoja wa Sovieti Bila shaka, au alichukuliwa na manowari ya Kichina.
Wengine walisema kwamba labda alijiua au amechukuliwa na UFO. Hiyo ilikuwa ni uvumi na nadharia za njama ambazo zimeongezeka baada ya Harold Holt, Waziri Mkuu wa 17 wa Australia, kupotea hiyo Desemba 17, 1967.
Harold Holt ni nani.
Kama nilivyosema awali Holt alikuwa Kiongozi wa Chama cha Uhuru, akiwa na umri wa miaka 59 tu alipopotea na bado alikuwa amefanya maisha yote katika huduma ya serikali ya Australia.
Baada ya kutumia miaka 32 Bunge, akawa Waziri mkuu wa Australia mnamo Januari 1966 kwenye jukwaa ambalo liliunga mkono Askari wa Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo, kazi yake kama waziri mkuu ilikuwa mfupi sana; alikuwa amekuwa waziri mkuu kwa muda wa miezi 22 tu na nafasi yake ilikatishwa na tukio la kuogelea.
Aliitumia Jumamosi ys Desemba 16 kutembelea na marafiki na familia na Jumapili, Desemba 17 asubuhi, alifungua kinywa, kisha alicheza na mjukuu wake na wakawasiliana na marafiki wengine waangalie chombo cha kutoka Uingereza na kwenda kwa kuogelea kwa muda mfupi.
Siku ya tukio.
Baada ya tukio la chombo cha kusafiria Holt aliwasiliana na marafiki zake ambao walijumuika kuogelea ambapo kwa mara ya kwanza, walimwona akiogelea bila shida.
Mawimbi yalipokua ya azidi, marafiki zake waligundua kuwa alikuwa katika taabu. Walipiga kelele ili arudi, lakini mawimbi yalimsukuma zaidi mbali na pwani. Dakika chache baadaye, alipotea, alikuwa amekwenda kusikojulikana.
Jaribio kubwa la utafutaji na uokoaji lilizinduliwa, lakini hatimaye utafutaji ulisitishwa bila ya kupata mwili wa Holt na siku mbili baada ya kupotea, Holt alidhaniwa amekufa na huduma ya mazishi iliandaliwa Desemba 22.
Malkia Elizabeth II, Prince Charles, Rais wa Marekani, Lyndon Johnson na wakuu wengine wa nchi walihudhuria mazishi ya Holt.