Dunia imejaa mambo mengi ya kupendeza na yasiyopendeza, lakini pia Dunia ina maajamu mengi ya kushangaza na mengine ni ya hatari zaidi. Kama ulikuwa unapanga kutembelea maeneo yote ya Dunia basi kuna sehemu nyingine inabidi ughairi kwani ni hatari kwako.

Zifuatazo ni sehemu hatari zaidi kutembelea Duniani kwani huko Mamlaka husika zimetoa onyo mara kadhaa ama usifike kabisa, ama uwe na wenyeweji au ufike lakini ukiwa unafahamu fuka kwamba lolote linaweza kukutokea.

Barabara ya kifo.

Barabara ya Yungas Kaskazini, hii inajulikana kama “Barabara ya Kifo” kwa sababu zote sahihi ambazo unaweza kudhani.

Kuendesha gari au kushuka kwa kurudi nyuma kwa maili 43 (kilometa 69) ni hatari sana kwa sababu ya ukungu, maporomoko ya ardhi, maporomoko ya maji na miamba inayoanguka mita 2,000 (610 mita) .

Hadi kufikia 1994, karibu madereva 300 walikufa, watu wakathibitisha jina la utani la barabara ya kifo na kuiweka kwenye orodha ya maeneo hatari zaidi kutembelea ulimwenguni.

Kisiwa cha Nyoka.

Kuna kisiwa kilicho karibu maili 25 kutoka pwani ya Brazil, ambapo hakuna mtu wa ndani ambaye anaweza kuthubutu kutembelea.

Upo uvumi kwamba mvuvi wa mwisho ambaye alipotea karibu na mwambao wake alipatikana akielea kwenye mashua yake siku chache baadaye, akiwa ameaga dunia .

Kisiwa hicho cha kushangaza kinajulikana kama Ilha da Queimada Grande, na ufikiqji wa hapo unaarifiwa kuwa ni hatari na Serikali ya Brazil imeharamisha mtu yeyote kutembelea.

Ziwa la Chumvi.

Unaambiwa hapa usiruhusu kuhadaiwa na wingi wa chumvi kando ya Ziwa Natron kwani ni moja ya maeneo yasiyofaa ulimwenguni.

Ziwa Natron lililopo kaskazini mwa Tanzania linaonekana kama ziwa la moto kwani viwango vya juu vya Natron (sodium carbonate decahydrate) hufanya maji yake kuchubua ngozi ya binadamu na macho na wakati mwingine kufikia kiwango cha ph zaidi ya 12.

Bonde la Kifo.

Ni Bonde la jangwa lililipo mpakani mwa California na Nevada likiwa na joto kali.

Lenyewe linajulikana kama moja ya maeneo yenye joto kali zaidi ulimwenguni.

Kuna majangwa machache pekee katika Mashariki ya Kati na Afrika, yanayokaribia joto kali wakati wa majira ya joto, yanayoweza kutoa ushindani kwa Bonde hili la Kifo.

Joto la wastani, pamoja na kiwango cha chini cha usiku, lilikuwa 108.1 ° F.

Kwa siku nne mfululizo, viwango vya juu vya kila siku vilifikia joto la 127 ° F, ambalo ni joto la juu kabisa lililorekodiwa.

Lango la kuzimu.

Hili ni Bwawa la Gesi la huko nchini Turkmenistan Darvaza likijulikana kama “Lango ya Kuzimu.”

Ni eneo la gesi asilia ndani ya pango la chini ya ardhi. Wataalamu wa jiolojia waliwasha moto kuzuia gesi ya methane kuenea, na imekuwa ikiwaka tangu mwaka 1971.

Iko katikati ya Jangwa la Karakum, karibu kilomita 260 kaskazini mwa mji mkuu wa Turkmenistan, karibu na kijiji cha Derweze, Ashgabat na sasa limekuwa eneo la utalii.

Benchikha amkataa mazima Chama
Van de Beek atimkia Ujerumani