Mahakama ya Wilaya ya Ulanga ya Mkoani Morogoro, imemuhukumu Mohamed Lihuka kutumikia kifungo cha miaka 20 jela, kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali bila kuwa na kibali.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Rancy Mhaya amesema Mtuhuniwa Lihuka amepatikana na hatia na atatumikia kifungo cha miaka 20 jela.
Mtuhumiwa huyo, alikamatwa Februari 2023 katika Kijiji na Kata ya Uponera kilichopo Wilayani Ulanga Morogoro, akiwa na vipande 87 vya nyama pori ya Nyati.
Alifikishwa katika kituo cha Polisi Mahenge na Machi 15, 2023 alipelekwa Mahakama ya Wilaya Ulanga na kushtakiwa kwa kesi ya kupatikana na nyara za Serikali.