Wakulima Zaidi ya 900 wa Ushirika wa Wakulima wadogo wadogo wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Mpunga Dakawa (UWAWAKUDA), waliopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wamegomea kuwasilisha hati ya Shamba namba 5/3 kwa Wizara ya Kilimo kwa kuhofia kunyang’anywa mashamba yao.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Umoja wa Wakulima hao, baadhi ya wakulima wamesema hawana imani na timu ya wataalam kutoka Wizara ya Kilimo waliofika hapo kwa lengo la kutaka kukabidhiwa hati hiyo bila kufuata utaratibu, ambapo Wakulima hao walikabidhiwa hati hiyo tangu mwaka 2012 na walianza kulima tangu mwaka 1974.

Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Said Hussein Nguya, akitoa salama za Serikali baada ya mjadala huo, alisema kuwa wao hawana taarifa rasmi za ujio wa wataalam hao.

Amesema, kama uongozi wa Wilaya wakati wote wataendelea kulinda maslahi ya Wananchi na hawapo tayari na hawatakubali Kwa namna yoyote maslahi ya Wananchi wa Mvomero yakatikiswa, hivyo suala hilo litakwenda ofisini na watalipima faida na hasara zake KWA wananachi wa Mvomero.

Ushirikiano: Vitu lazima vitokee: Makamba
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 21, 2024