Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amekagua itekelezaji wa kazi ya uchimbaji Visima vya Maji inayofanywa na Magari ya Mitambo ya Uchimbaji, katika eneo la milima ya Kilimarondo Wilayani Nachingwea inayofanyika mikoa yote nchi nzima.

Waziri Aweso ameshuhudia Gari maalumu la Mkoa wa Lindi likifanya kazi baada ya kuwa kupaki muda mrefu na kupeleka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutoa maelekezo mahususi.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso ametoa maelekezo mahususi nchi nzima yatakayosimamiwa na Meneja wa Uchimbaji Visima na ujenzi wa Mabwawa Mhandisi Ndele Mengo aliemteua hivi karibuni.

Aidha, Amesisitiza kuwa atafanya kazi ya kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu utendaji kazi na ufanisi wa mitambo hiyo na kutoa maagizo magari yote ya uchimbaji kutoondolewa na kubaki kwenye mikoa yaliopo kabidhiwa.

LAAC yataka usimamizi utekelezaji miradi 'force account'
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 28, 2024