Scolastica Msewa, Mkuranda – Pwani.

Baadhi ya Madiwani viti maalumu na Katibu wa UWT Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Nurati Mkandawile wamefanya usafi wa kuzunguka viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Mkuranga kama ishara ya kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa.

Hafla hiyo fupi ilifanyika katika Ofisi ya UWT Wilayani humo, ambapo pia walikata keki ya kumtakia maisha marefu yenye heri Rais Dkt. Samia na kuwahusisha jumuia ya Wazazi Wilaya.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, Nurati aliwataka Madiwani hao kwenda kuhamasisha akinamama kuchukua fomu za kuombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji.

Aidha, aliwataka Madiwani hao wa Viti maalumu kwenda pia kutembelea na kufanya mikutano na kuzungumza na akinamama kusikiliza kero za Wanawake katika Kata ,mitaa vitongoji, vijiji na mitaa yao.

Naye Diwani Viti maalumu, Fatuma Kingwande alisema Madiwani hao wapo tayari kukihudumia Chama na Wanachama wake, ili CCM kikakubalike kwa Wanachama na kwa Wananchi pia.

Upendo, furaha vyatawala 'Polisi Family Day' Moro
Bunge marathon kukusanya fedha ujenzi Shule maalum