Mbunge wa Magarini Nchini Kenya, Harrison Kombe amekosoa hatua ya serikali kupiga marufuku disko matanga, kama njia ya kupambana na mimba za utotoni.

Hatua hito inatokana na tamko la Serikali la kupiga marufuku disko hilo la kukesha (Kigodoro), katika kaunti ya Kilifi, wakidai unachangia mimba nyingi na kuharibu ndoto za wasichana wengi kimaisha.

Mbunge wa Magarini Nchini Kenya, Harrison Kombe.

Kombe amesema, zipo sababu zingine zinazosababisha mimba za utotoni, na sio disko matanga kama inavyosemekana, huku akiitaka idara ya usalama kuondoa marufuku hiyo.

Hata hivyo, Baadhi ya Wananchi wameungana na Mbunge huyo wakisema mimba inaweza kuingia popote na kwamba Serikali inahitaji kufikiria zaidi ya hapo juu ya hatua stahiki na si kuzuia burudani hiyo.

Ukiukwaji kanuni za maadili: Madaktari tisa hatiani
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 10, 2024