Beki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Dylan Batubinsika amesema kuwa atayachukulia kawaida matokeo ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ivory Coast.

Beki huyo wa St. Etienne ya Ufaransa amezungumza baada ya timu yake kufungwa kwa Penati 6-5 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa kusaka nafasi ya tatu na nne juzi Jumamosi (Februari 10).

“Nimefurahishwa na taji hili. Namshukuru Mungu kwa jambo hili. Nafikiri tunaweza kujivunia mashindano yetu. Tulicheza vizuri na safari yetu ilikuwa poa. Wachache ndio walifikiria kama tunaweza kufikia hatua hii na hii inatujengea hatima nzuri, “amesema beki huyo.

Licha ya timu hiyo kukosa medali ya shaba, beki huyo amesema kuwa inabidi kuyachukulia kawaida kwani matokeo hayo na mashindano yamewafunza mengi.

“Nitakumbuka mazuri tu kutoka katika safari yetu hii ya mashindano haya. Kumbukumbu yangu kubwa inabaki katika ushindi wetu dhidi ya Misri. Mchezo ulikuwa dhidi ya kikosi bora kabisa.”

De Jong kucheza England 2024/25
Kasi utekelezaji Miradi ya Maji yaifikia Turiani