Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemhakikishia Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Conar na ujumbe wake kuwa, Serikali ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Nutri-Sun Limited kutoka Uingereza katika kukamilisha mradi wa kiwanda cha kuchakata mwani

Kiwanda hicho kilichopo Chamanangwe, Pemba, kukamilika kwake kutawanufaisha kwa kurahisisha kupata soko la uhakika.

Katika salamu zake, Balozi Conar amemweleza Dkt. Mwinyi kuwa mipango ya kupata mashine na teknolojia ya kuchakata mwani imekamilika, hivyo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024 kiwanda hicho kitaanza kuzalisha “Carrageenan” ambayo itatatumika kwa matumizi ya viwanda vya chakula na matibabu.

Naye Marisa Drew kutoka wa Standard Chartered alimhakikishia Rais Dkt. Mwinyi upatikanaji endelevu wa fedha ambazo zitatumika kununulia mashine na zao la mwani.

Kiwanda hicho, pia kitawawezesha wakulima wa mwani hasa wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi.

REB yatarajia matokeo kuwatumikia Wananchi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 20, 2024