Takriban Watu tisa wamefariki dunia, huku wengine 30 wakijeruhiwa, kufuatia ajali ya  barabarani iliyohusisha gari ya abiria maarufu kama matatu Nchini Kenya.

Ajali hiyo, imetokea Februari 26, 2024 majira ya alasiri karibu na soko la Katangi katika barabara ya Kitui-Machakos kaunti ya Machakos.

Polisi Nchini humo imesema kqti ya watu hao tisa waliofariki, yumo mtoto wa umri wa miaka 9 na wote walifariki papo hapo.

Inaarifiwa kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya Dereva wa matatu ya abiria waliokuwa wakisafiri, ambayo pia ilikuwa ikisafirisha makaa, kushindwa kulidhibiti gari hilo.

Dkt. Yonazi afungua Kikao kazi kuhuisha Sherehe za Kitaifa
Kodi ya Sukari yaondolewa Zanzibar