Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kwenye bidhaa ya sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi katika ziara yake maalumu ya alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Amewasisitiza Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar(ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.

Ajali: Daladala yauwa tisa, 30 majeruhi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 27, 2024