Klabu ya Chelsea ina matumaini ya kuwauza baadhi ya mastaa wa kikosi cha kwanza katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Nyota hao ni pamoja na beki Trevoh Chalobah mwenye umri wa miaka 24, na Mshambuliaji Armando Broja mwenye umri wa miaka 22.

Mastaa hao wamekuwa wakihusishwa kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa sababu hawapati nafasi za kutosha katika kikosi cha kwanza cha matajiri hao wa jiji la London.

Mbali ya mastaa hao pia kuna uwezekano wa kiungo Conor Gallagher mwenye umri wa mika 24 na beki Marc Cucurella mwenye umri wa miaka 25 wakaondoka katika dirisha lijalo.

Kwa upande wa Chalobah amekuwa akihusishwa kutua kwa mabingwa wa Soka nchini Ujerumani Bayern Munich.

Chelsea pia inawauza wachezaji hao, kwa sababu inataka kuboresha timu kwenye dirisha lijalo, ambapo inaonekana kuwa ngumu kusajili kutokana na sheria za matumizi ya kifedha na mwaka jana ilitumia pesa nyingi bila ya kuuza.

ABU mbinu mpya uandaaji Vijana wabobevu sekta ya Madini
Fabrice Ngoma: Mechi ipo mikononi mwetu