Mzee wangu Ali Hassan Mwinyi ni miongoni mwa Viongozi waliokiwa wamejaaliwa hekima na busara nyingi kati ya wale waliopata kutokea hapa nchini.

Na katika utawala wake, alionesha umahiri mkubwa katika kutumia lugha ya Kiswahili kufikisha ujumbe kwa watu wake tena kwa lugha nyepesi na mara nyingi kwa kutumia tungo za kifalsafa.

Kwenye moja ya hotuba zake alizowahi kuzitoa wakati wa utawala wake, Mzee Mwinyi alizungumzia dhana ya Demokrasia na uchumi wa soko huru.

Katika hili, aliangazia juu ya umuhimu na changamoto zake kwa kutolea mfano wa Chumba na Dirisha.

Alisema, “kama chumba hakina hewa na mwanga wa kutosha basi ni vema ukafungua dirisha. Lakini, kufungua dirisha kuna maana pia ya kuruhusu nzi na mbu kuingia chumbani kwako.”

Utafanyaje? unahitaji hewa lakini Mbu na Nzi nao wana yao, hapo nadhani haitakuwa vema kulifunga tena dirisha.

Bila shaka cha muhimu ni kwamba itakupasa utafute dawa ya kuulia Nzi na Mbu huku ukiruhusu hewa safi iingie chumbani mwako.

Hizi ni busara zenye funzo ndani yake, ni wazi kwamba huwezi kuyatenganisha maanikio na changamoto, na ushujaa huja kwa mapambano, acha tuyaishi mema ya Mzee Mwinyi.

Ummy: Watumishi wa mikataba wajiriwe kwa mapato ya ndani
Makala: Maisha ya Mwanadamu ni Hadithi tu