Jamii ya wafanyabiashara ndogo ndogo mkoani Iringa (Machinga) wametakiwa kuacha vitendo vya uchochezi vinavyopelekea kutokea kwa migogoro kwenye jamii.

Akizungumza kwenye kikao kilichohusisha wafanyabiashara hao na uongozi wa Mkoa wa Iringa hii leo Machi 3, 2024, Kamanda wa polisi mkoani humo, Allan Bukumbi amekemea vikali vitendo hivyo vinavyochochea migomo na vurugu na wakati mwingine kusababisha machafuko.

Amesema, Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu au kikundi chochote kitakachobainika kuendesha vitendo hivyo vya kichochezi ambavyo kisheria ni kosa la jinai.

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 4, 2024
Ujumbe wa Rais Dkt. Mwinyi kwa Rais Dkt. Samia