Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega tangu Mzee Mwinyi alipoanza kuugua mwezi Novemba alipopelekwa Uingereza kwa matibabu.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Machi 3, 2024 katika hitma na Dua Maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ilyoandaliwa na Rais Samia katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Aidha, amewashukuru pia Madaktari wa Hospitali ya Mzena kwa kazi kubwa waliyoifanya kujaribu kuokoa maisha ya Mzee Mwinyi pamoja na Masheikh, Waalimu, Ndugu, Marafiki na wananchi kwa dua nyingi walizomuombea Mzee Mwinyi kwa kupindi chote alichokuwa akiugua na baada ya kufariki.

Machinga watakiwa kuacha uchochezi Mtandaoni
MAKALA: Nautafakari Uzee