Mkurugenzi Mkuu Taasisi  ya  Utafiti wa  Wanyamapori  Tanzania – TAWIRI, Dkt. Eblate  Ernest Mjingo  amesema teknolojia  mbalimbali  zimerahisisha  tafiti za  Wanyamapori nchini kufanyika kwa wakati na kwa usahihi na kwamba wameanza rasmi zoezi la kuwatoa tembo mikanda ya visukuma mawimbi (GPS Collars ) katika Wilaya za Longido, Hanang, Babati, Monduli ambapo kuna shoroba za wanyamapori zilizopitiwa na mradi wa Njia ya Umeme ya Msongo wa kV 400 wa Kenya – Tanzania Power Interconnection Project (KTPIP).

Akizungumza Wilayani Longido, Dkt.Mjingo ameeleza kuwa katika Mradi wa KTPIP unaokatiza maeneo ya Shoroba za wanyamapori za Tanganyeeti na Laasarack Wilayani Longido, Ushoroba ya Kwakuchinja Wilayani Babati, Mswakini chini Wilayani Monduli na Pori la akiba la Swagaswaga, TAWIRI imefanya tafiti na kuishauri Serikali kupitia TANESCO ili kuwa na uhifadhi endelevu nchini..

Amesema, miongoni mwa teknolojia  zinazotumika katika tafiti za wanyamapori ni pamoja na matumizi ya tekinolojia  ya akili mnemba, kuchakata takwimu na uchambuzi wa picha katika zoezi la kuidadi wanyama (sensa), teknolojia ya  mikanda ya visukuma mawimbi, kufuatilia mienendo ya wanyamapori, matumizi ya ndege zisizo na Rubani rubani kutatua changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Dkt. Mjingo amesema, matumizi  ya helikopta/ndege kuwafuatilia wanyamapori kwa matibabu au kuwarejesha wanyama  maeneo ya hifadhi, kamera za kutega (camera  trap) kubaini  aina ya wanyamapori waliopo katika  maeneo mbalimbali na changamoto za uhifadhi na tekinolojia  ya vinasaba (DNA) kutambua afya ya uzazi wa wanyamapori kwenye mifumo ikolojia mbalimbali.

Awali, kabla ya matumizi ya teknolojia kulikuwa na ugumu katika kufanya  tafiti za wanyamapori baadhi ya maeneo kwani iliwalazimu watafiti kutumia muda mrefu kufanya tafiti, kutumia gharama kubwa, usalama  mdogo.

Dkt. Msonde aagiza utolewaji mafunzo mfumo wa NeST
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 4, 2024