Mahakama ya Juu nchini Marekani imemsafishia njia rais wa zamani wa Taifa hilo Donald Trump, kuwania urais katika uchaguzi ujao baada ya kutoa uamuzi unaoyazuia majimbo ya nchi hiyo kuliondoa jina lake kwenye kura za mchujo.

Katika uamuzi huo wa pamoja uliotolewa Machi 4, 2024 majaji 9 wa mahakama hiyo wamebatilisha uamuzi wa mahakama kuu ya jimbo la Colorado uliozuia jina la Trump kuwemo katika kura za mchujo za jimbo hilo.

Desemba 2023, Mahakama ya Colorado ilitoa hukumu kwamba Trump hatoruhusiwa kuwania urais kwenye jimbo hilo kwa msingi kwamba alihusika kuchochea uasi dhidi ya Serikali mnamo Januari 6, 2021.

Hata hivyo, Mahakama hiyo ya Juu imesema majimbo ya Marekani hayana nguvu kisheria ya kuwaondoa wagombea kwenye kinyang ányiro cha uchaguzi, huku Trump akiutaja uamuzi huo kuwa ushindi mkubwa kwa Marekani.

Simulizi: Njia waliyotumia wazazi wangu ili nifaulu masomo
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 5, 2024