Shirika la Chakula na Kilimo Duniani – FAO, limesema Wakulima Wanawake na familia za Vijijini katika nchi maskini duniani, ndio waathirika wakubwa wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Kupitia ripoti yake ya hivi karibuni ya hali ya hewa isiyo ya haki, FAO imeeleza kuwa Wanawake hao wanabaguliwa pindi wanapojaribu kutafuta vyanzo vingine vya mapato kutokana na hali hiyo.

FAO imebaini kuwa familia nyingi za Vijijini zinazoendeshwa na Mwanamke hupoteza kwa wastani asilimia 8 ya mapato yake wakati wa joto kali na asilimia 3 zaidi wakati wa mafuriko, ukilinganisha na familia zinazoongozwa na wanaume.

Aidha, ripoti hiyo pia imeonya ikiwa tofauti kubwa zilizopo, katika uzalishaji wa Kilimo na mishahara baina ya Wanaume na Wanawake hazitoshughulikiwa, huenda mabadiliko ya hali ya hewa yakaongeza tofauti wakati ujao.

Ubovu wa miundombinu: Serikali yaipa siku nne TANROADS
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 6, 2024