Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.

Watu watatu wameuwawa kikatili na wengine wanne kujeruhiwa akiwemo mama mwenye ujaumzito wa miezi 7, huku mtuhumiwa wa mauaji hayo Ahita Dahachi (42), akidaiwa kuwa na matatizo ya Afya ya akili.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara SACP, George Katabazi amesema tukio hilo limetokea Machi 13, 2024 katika Kata ya Sirop Wilayani Hanang’.

Waliouwawa ni Mama mzazi wa mtuhumiwa, Mama wa jirani ambaye ni mjamzito wa miezi 7 pamoja na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja.

Kamanda Katabazi amesema, chanzo Cha tukio hilo ni matatizo ya Afya ya akili aliyokuwanayo mtuhumiwa Dahach na mpaka sasa anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi na mahojiano zaidi.

Simba SC, Al Hilal zamuwania Dube
Uvamizi: Maeneo Viwanja vya Ndege yapate hati miliki