Droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inatarajiwa kufanyika baadae leo Ijumaa (Machi 15) mjini Nyon, Uswisi ambapo macho na masikio yote yatakuwa huko kujua nani atapangwa na nani.

Bingwa mtetezi Man City alitinga hatua ya Robo Fainali baada ya kuwaondoa Copenhagen kwa jumla ya mabao 6-2.

Arsenal iliingia kiugumu kwa kuishinda Porto kwa Penati mapema juma hili baada ya matokeo ya jumla ya 1-1.

Arsenal na Man City ndio timu pekee kutoka England ambazo zimesalia kwenye hatua hiyo.

Hispania ndio nchi iliyoingiza timu nyingi zaidi kwenye hatua hiyo katika michuano ya mwaka huu ikifanikiwa kuziingiza Real Madrid, Atletico Madrid na FC Barcelona ambazo zote zilimaliza hatua ya makundi zikiwa vinara.

Ujerumani pia imeingiza timu mbili sawa na England ambazo ni Bayern Munich na Borussia Dortmund ambapo kumekuwa na utabiri kwamba Mshambuliaji wa The Bavarian, Harry Kane huenda akarejea tena nchini England akiwa na Munich kutokana na Droo hiyo.

Ufaransa imeingiza timu moja tu, PSG, ambayo kwenye hatua ya makundi ilimaliza nafasi ya pili chini ya Dortmund na kwenye hatua ya l6 bora iliitoa Real Sociedad.

Katika siku za hivi karibuni timu hii imekuwa na migogoro na staa wao Kylian Mbappe ambaye anahusishwa kuondoka mwisho wa msimu huu 2023/24.

Gamondi: Sina uhakika wa kutwaa ubingwa
Simba SC, Al Hilal zamuwania Dube