Takribani Watu wameaga dunia na wengine 38 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara kuu ya Herat-Kandahar, Wilayani Greshk, Mkoa wa Helmand uliopo kusini mwa Afghanistan.

Taarifa ya Polisi wa eneo hilo imesema chanzo cha ajali hiyo ni basi la abiria kugongana na pikipiki na kisha dereva wa basi kupoteza udhibiti wa gari lake na kugonga lori la mafuta hivyo kusababisha moto mkubwa.

Polisi wamezidi kufafanua kuwa, Watu 11 wapo katika hali mbaya na wanapatiwa matibabu katika hospitali mkoani humo.

Ajali za barabarani zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara nchini Afghanistan, ambako maelfu ya watu hufariki kila mwaka kutokana na ubovu wa barabara, matengenezo hafifu pamoja na ukosefu wa umakini katika uendeshaji wa vyombo vya moyo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 18, 2024
Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa shughulikieni migogoro ya ardhi