Februari ya mwaka 2021, wapendanao kutoka mji wa Kharkiv nchini Ukraine Viktoria Pustovitova (29) na Alexander Kudlay (33), waliamua kujifunga minyororo kwa zaidi ya miezi mitatu, ili kujaribu uimara wa mahusiano yao na kama ishara ya kudumisha mapenzi yao.

Alexander ndiye aliyetoa wazo la kujifunga pingu pamoja na mpenzi wa Viktoria ambaye alimuambia kuwa anataka kuachana naye hivyo kutafuta mnyororo huo na kujifunga kwa siku 123, wakifanya kila kitu pamoja kuanzia mapumziko, kula kunywa kuoga na hadi manununuzi ya mahitaji muhimu.

Jambo hili liliathiri shughuli zao kwani Alexander aliweza kuendelea kufanya kazi kama muuzaji wa magari akiwa na mpenzi wake lakini wateja hawakupendezwa, huku kwa upande wa Viktoria yeye ilimbidi aache kazi yake ya kutengeneza kope za bandia kwa sababu wateja wake hawakuridhika kuwa karibu sana na mwenzi wake.

Hata hivyo, wawili hao walivunja rekodi ya Kiukreni na ya Ulimwengu kwa muda mwingi waliotumia kujifunga mnyororo huo pamoja kama wapenzi na walikuwa wameapa kubaki hivyo hadi watakapofunga ndoa licha ya kwamba walikuwa bado hawajachumbiana rasmi.

Wakiwa katika kifungo hicho cha hiari, walizungumza mengi ikiwemo mipango ya kuuza mnyororo wao kwa Dola 3 milioni kwenye mnada wa Kimataifa, ili kuchangia sehemu ya fedha kama hisani na kuweka zingine kwa matumizi yao ya kibinafsi.

Waswahili husema hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, hatimaye siku ya kifungo huru kutamatika ilifika na Mnyororo huo hatimaye ulikatwa na wataalamu wa kukata vyuma huko Kyiv kwenye mnara wa Unity, na mara ulipokatwa Bibie Viktoria alipiga kelele akasema, ‘Hooray’ nataka kuishi maisha yangu ya kujitegemea na kuwa kama mtu huru. Hatimaye niko huru.”

Wakati Victoria akifurahia, Alexander yeye alitumia muda huo kuwashukuru wafuasi wao ambao walikuwa wakifuatilia safari yao isiyo ya kawaida kwenye mitandao ya kijamii akisema, “asanteni nyote kwa kutuunga mkono. Tazama, sasa hatuna mnyororo tena. Tulikuwa na furaha na sasa tuna furaha zaidi kwa kuwa na uzoefu huu katika maisha yetu.”

Alipomaliza Victoria naye akasema, “Tunajaribu sana kutokuza migogoro. Ninapambana na kusikia kelele ninapopika, au kwenye simu. Na sipendi kutumia muda mwingi karibu na kioo kila asubuhi kisa kuna mtu nipo nae pembeni yangu hili lilinichosha na sasa najihisi kuwa huru zaidi, hakika nipo huru.”

Baada ya mabishano ya muda mbele ya wanahabari, Alexander alichapisha kwenye mtandao wake kuwa “Rasilimali zetu zimekauka. Tunahitaji kupumzika tunahitaji kuachana. Tunahitaji kuanzisha upya. Tunapoenda kufanya ununuzi, tunaanza upya na furaha, tunamalizia kama ndimu zilizokamuliwa.”

Wapenzi hawa wakaachana rasmi ndani ya masaa manne tangu kujifungua minyororo.

Dkt. Gema: Kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya mwili, Meno
Dkt. Biteko: Nia ya Rais ni kuona Wananchi wanapata huduma bora