Beki wa kati wa Simba SC, Che Fondoh Malone, amesema utulivu wa kambi ya siku saba waliyoiweka Zanzibar ina maana kubwa kwao katika maandalizi ya mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Machi 29, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Malone amesema wanaenda kucheza mechi kubwa ya maamuzi hivyo ni muhimu kwa wachezaji kupata sehemu tulivu isiyokuwa na mwingiliano mkubwa wa watu kwa ajili ya kutengeneza mipango yao ya kuivaa Al Ahly.

“Tunahitaji kambi tulivu ambayo hatutapata bugudha, hatua tuliyopo ni hatua ngumu sana tunaenda kukutana na bingwa mtetezi hivyo ni mechi kubwa sana.

“Hivyo tunahitaji maandalizi ya hali ya juu na kuwaheshimu, kuja hapa visiwani Zanzibar kuna maana kubwa kwetu kwani tunapata nafasi wachazaji kukaa pamoja kwa ajili ya kujadili mambo mengi ya jinsi ya kucheza mchezo huu mkubwa,” amesema.

Amesema kocha mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha anaendelea kusuka mipango yake, hivyo wao kama wachezaji wanaendelea kupokea maelekezo ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo ujao.

“Hii itakuwa mara ya tatu kukutana nao, tulikutana kwenye Afrika Football League (AFL) walituondoa lakini safari hii kila timu itakuja kivingine hivyo haitakuwa rahisi,” amesema.

Conte kumfuata Harry Kane Bayern Munich
Dani Alves apata ahuweni Hispania