Baada ya mapumziko ya siku saba, Mtibwa Sugar imerejea tena mzigoni, kwa lengo la kujiandaa kuziwinda alama 30 za michezo 10 iliyosalia msimu huu 2023/24.

Nahodha wa timu hiyo, Oscar Masai amesema inabidi mechi 10 zilizosalia wazicheze kimkakati zaidi, ili kutumiza malengo waliojiwekea na kuinusuru timu yao isishuke daraja.

“Tusichopenda ni kuona timu inashuka daraja na tutahakikisha mechi 10 zilizobaki tunafia uwanjani kutafuta pointi tatu, sisi wachezaji tuko imara na tayari kuipambania Mtibwa.”

Lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Zuberi Katwila amesema wachezaji watakuwa vizuri kisaikolojia kuliko walivyoondoka.

Tangu walipomaliza mechi ya Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar waliyotoa suluhu Machi 12, wachezaji walipewa mapumziko ya juma moja na tayari wamerudi kambini.

Timu hiyo kongwe nchini haijawa na matokeo mazuri licha ya kufanya mabadiliko kwenye Benchi la Ufundi na hadi sasa wapo mkiani kwa alama l6 baada ya michezo 20.

Mtibwa Sugar ilianza msimu na Habibu Kondo ambaye baadae alitemwa baada ya mabosi kutoridhishwa na matokeo na kumkabidhi mikoba Katwila ambaye alitokea Ihefu FC.

Katwila amesema kwa muda waliotoa mapumziko kwa mastaa, anaamini kila mmoja amebadilika kisaikolojia hivyo wanapoanza mazoezi ataisuka upya timu hiyo na kung’atuka mkiani.

Tunajua ligi ni ngumu kwa sababu tumeachana pointi chache, hatuna matokeo mazuri ila lolote linawezekana, benchi la ufundi tunaendelea kutengeneza upya muunganiko na kusahihisha makosa ya jumla,” amesema kocha huyo.

Bahati mbaya kwa Sven Botman
Robinho ahukumiwa miaka tisa