Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemteua mwanaye Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Majeshi hali ambayo imeibua mshangao na mjadala miongoni mwa jamii ya Nchini Uganda na kwingineko Duniani.

Mamlaka hayo ya Mkuu wa Majeshi yalifanyiwa mageuzi na kutangazwa mwezi uliopita (Februari 2024), ambapo Wadadisi wa mambo na Wanasiasa, wanasema uteuzi wa Muhoozi ulipangwa kitambo.

“Hii si ajabu kwamba sasa jambo limefanyika katika kipindi cha kuelekea msimu wa uchaguzi mkuu. Nchi hii ilikwisha tekwa Serikali sasa imetekwa, kwani hata Majeshi yametekwa na familia,” alisema Kiongozi wa upinzani Nchini Uganga, Dkt. Kizza Besigye.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa kuteuliwa kwa Jenerali Muhoozi ni mpango wa Museveni kumdhibiti mwanaye ambaye alitangaza kugombea urais kwa kuzindua vuguvugu la kumpigia kampeni.

Wachezaji Young Africans wamshangaza Gamondi
Mashabiki Chelsea wamchana mmiliki