Idara ya usalama ya Urusi imesema zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia tamasha la muziki lililofanyika karibu na mji mkuu Moscow.

Tukio hilo, linadaiwa kutekelezwa na washambuliaji watano waliokuwa wameficha nyuso zao, ambao walifyatua risasi kwa watu waliokuwa kwenye tamasha lililofanyika ukumbi wa Crocus, katika kitongoji cha kaskazini magharibi cha Krasnogorsk.

Hili linakuwa ni moja ya shambulizi baya zaidi nchini Urusi tangu kuvamiwa kwa shule ya Beslan mwaka 2004 Nchini humo, ambapo zaidi ya watu 330, nusu kati yao wakiwa watoto, waliuawa.

Tayari kundi la kigaidi la ISIS limekiri kuhusika na shambulizi hilo kupitia ujumbe mfupi uliochapishwa kwenye mtandao wa Telegram na Chombo cha Habari wanachokitumiwa kurusha taarifa zao cha Amaq.

Simulizi: Nilivyokimbiwa kisa sina pesa, anajuta
Mshukiwa mauaji ya Wazee Kaloleni adakwa