Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema Dunia tuliyopo sasa ingekua na nusu ya Viongozi Wanawake basi ingekua bora zaidi ya ilivyo hivi sasa.

Prof. Mkumbo ameyasema hayo kwenye kilele cha utoaji wa tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 zilizoandaliwa na Clouds media Group kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam, na kusema ni lazima kumuinua Mwanamke kama tunataka Dunia iwe bora zaidi.

Kwenye eneo lingine Prof. Mkumbo amekazia maneno yaliyosemwa na mshindi wa tuzo ya Heshima Mama Getrude Mongella ya kuwa Rais Samia aachwe ikitokea kuna mwingine asubiri miaka ijayo, kwenye kukazi hili Profesa Mkumbo amesema ‘Naungana na Mama Mongella, kazi ya mwaka kesho imeshaisha. Tutakua na uchaguzi wa Wabunge na Madiwani lakini Rais tayari tunaye’ – Kitila Mkumbo.

Malkia wa Nguvu ni tuzo zinazotolewa kila mwaka kwa mwaka wa nane mfululizo zikiandaliwa na kutolewa na Clouds Media Group ambapo kwa mwaka huu 2024 aina 9 zimetolewa kutoka kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Ubunifu na Huduma za Jamii.

Putin: Aliyewaagiza, waliotekeleza wote kukiona
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 24, 2024