Asila Twaha, Mwanga.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Hosptali ya Wilaya pamoja na kituo cha afya Kirya katika halmashauri hiyo.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati, Ester Bulaya amyaesema hayo baada ya kukagua miradi hiyo na kutoridhishwa utekelezaji wa miradi hiyo ambayo mpaka sasa imekamilika kwa asilimia 50.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miradi hiyo lakini Halmashauri hiyo bado inasuasua utekelezaji wake ambapo baadhi ya majengo bado hayajakamilika wakati ilishapewa zaidi sh. bilioni 2.

“Halmashauri nyingine wamepewa 1.8 wapo katika hatua nzuri ya utekelezaji na kuna majengo yameshakamilika na mengine yameanza kutumika kutoa huduma ila Halmashauri ya Mwanga haijakamilisha” amesema taarifa inasema kuna vifaa stoo vya zaidi ya shs. milioni 200 na hakuna hata jengo moja lililokamilika kwa asilimia 100, ” alihoji Bulaya

Pia amekerwa kutokufuatiliwa kwa vifaatiba na dawa MSD na Serikali ilishatoa pesa shs. bilioni 1.1 ” tumesikia hivi karibuni vimefika vifaa vya milioni 100 tu kisa mmesikia Kamati inakuja ” watendaji timizeni wajibu wenu” amewasisitiza

Ofisi ya Rais -TAMISEMI pia imetakiwa kabla hawajatoa na kushughulikia fedha walizotakiwa waongeze kwa Halmashauri sh. milioni 300 kwanza wafanye tathmini na ufuatiliaji wa kiasi cha fedha ambacho kishatumika zaidi ya sh. bilioni 2 katika kutekeleza mradi huo.

Kamati, imemtaka CAG afanye uhakiki wa vifaa vilivyopo stoo vya kiasi cha shs. milioni 202 na kuwasilisha taarifa kwa Kamati kabla ya tarehe 28 Machi, 2024.

Aidha, Kamati pia imemtaka Mkurugenzi awasilishe taarifa kwa CAG kwa ajili ya uhakiki kibali cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kilichoiruhusu Halmashauri kutekeleza mradi kinyume na miongozo ya utekelaji wa mradi

Utekelezaji wa Miradi: Sheria za manunuzi zifuatwe - Kamati
Dkt. Rwakatare atunukiwa Shahada udaktari wa heshima