Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Chuo kikuu cha nchini Marekani cha All Nations Christian Church International University kilichopo Texas Nchini Marekani (ANCCI), kimemtunukia Udaktari wa heshima (PhD) Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Wazalendo Huru, Dkt. Mohamed Mwampogwa kwa utumishi wake anaoufanya kwa jamii.

Sherehe ya kutoa shahada hiyo kwa watu mbalimbali imefanyika mjiji Kibaha kwa Mbonde Mkoa wa Pwani, ambapo Mwakilishi wa chuo hicho Menya, Prof. Purity Gatobu alitunuku Shahada hizo.

 

Akizungumza mara baada ya kutunukiwa Shahada hiyo, Dkt. Mwampongwa ameshukuru Chuo Kikuu hicho kwa kutambua mchango wake kwa jamii kitu ambacho kimempa ari ya kuendelea kutumikia jamii kwa kutoa msaada mbalimbali.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo huru Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Mkoa wa Pwani, Hadija Juma amesema Kila kiongozi katika nafasi yake anatakiwa kutatua changamoto na kero za Wananchi.

Amesema, jukwaa hilo litaendelea kuhudumia Wananchi kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Maendeleo katika jamii.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 25, 2024
Hatma ya Wanasenegal katika mikono yao hii leo