Taifa la Senegal linafanya uchaguzi wa rais hii leo siku ya Jumapili Machi 24, 2024 baada ya kampeni za majuma kadhaa zilizotanguliwa na machafuko, kufuatia tangazo la hapo kabla la kuahirishwa uchaguzi huo.

Amadou Ba na Bassirou Diomaye Faye  wanaochukuliwa kuwa washindani wawili wakuu katika uchaguzi ulio wazi zaidi katika historia ya Senegal huru, walionesha nguvu zao kabla ya siku ya mwisho wa kampeni, Ijumaa Machi 22, 2024.

Baada ya wagombea wawili kujitoa katika kinyang´anyiro hicho dakika za lala salama, uchaguzi huo umesalia na wagombea 17 wanaowania kurithi kiti cha urais kutoka kwa Macky Sall.

Mshindi wa uchaguzi huo atakuwa na kibarua kikubwa cha kuitoa nchi hiyo kipindi cha msukosuko kilichoshuhudiwa miaka ya hivi karibuni lakini kuweka mpango wa kuinufisha Senegal kutokana na mapato ya nishati ya mafuta na gesi yanayotazamiwa kuanza kupatikana.

Siku ya Ijumaa, wagombea wa kiti cha urais walifanya mikutano ya mwisho ya kampeni zilizofanyika kwa kipindi kifupi na bila matayarisho ya kutosha kutokana na sintofahamu ya kuahirishwa kwa uchaguzi.

Udaktari wa heshima wamfuata Dkt. Mwampogwa Kibaha
Utekelezaji wa Miradi: Sheria za manunuzi zifuatwe - Kamati